Vitate, Vitawe na Visawe


VITATE, VITAWE NA VISAWE
Kitengo Msamiati
MASOMO
Prev N/A
Next Tarakimu
Baadhi ya maneno ya Kiswahili yanaweza kuwa na maana sawa, maana zaidi ya moja au matamshi yanayotatiza. Vikundi hivi vitatu ni:
 1. Vitate - maneno yanayotatiza kimatamshi. ⇒ Vitate hutatiza kimatamshi
 2. Vitawe - maneno yenye maana zaidi ya moja. ⇒ Vitawe hugawanywa kwa matawi au maana zaidi
 3. Visawe - maneno tofauti yenye maana sawa. ⇒ Visawe huwa na maanasawa ''

Vitate

Maneno yanayotatiza kimatamshi.

 1. ndoa na doa :
  1. ndoa ⇒ kuungana kwa watu wawili na kuishi pamoja kama mume na mke
  2. doa ⇒ alama ya uchafu, kasoro au dosari
 2. baba na papa :
  1. baba ⇒ mzazi wa kiume
  2. papa ⇒ mnyama wa baharini
 3. fua na vua :
  1. fua ⇒ osha nguo, tengeneza vyuma
  2. vua ⇒ shika samaki kutoka majini; toa nguo
 4. faa na vaa :
  1. faa ⇒ inayostahili, inayopaswa
  2. vaa ⇒ weka nguo juu ya mwili
 5. ngoma na goma :
  1. ngoma ⇒ ala ya muziki itoayo sauti inapopigwa
  2. goma ⇒ acha kufanya kazi
 6. shinda na shida :
  1. shinda ⇒ ongoza katika makabiliano, mashindano
  2. shida ⇒ taabu au matatizo
 7. shindano na sindano :
  1. shindano ⇒ makabiliano baina ya watu wawili au zaidi ili kutambua atakayeongoza
  2. sindano ⇒ kifaa kinachotumika kushonea vitu
 8. pinga na piga :
  1. pinga ⇒ kutokubaliana na jambo fulani
  2. piga ⇒ kugonga au kuchapa
 9. fahali na fahari :
  1. fahali ⇒ ng'ombe wa kiume. pia ndume
  2. fahari ⇒ kujivunia, furaha
 10. haba na hapa :
  1. haba ⇒ kisichokuwa kingi
  2. hapa ⇒ mahali karibu

Vitawe

Mano yenye maana zaidi ya moja
 1. paa :
  1. kwea (enda juu)
  2. mnyama wa porini anayefanana na mbuzi
  3. sehemu ya juu ya nyumba
 2. shinda :
  1. kaa au ishi mahali/wakati fulani
  2. ongoza katika shindano
  3. tupu
 3. kaa :
  1. sehemu yenye moto ya kuni
  2. mnyama wa majini
  3. keti chini
  4. kuwa mahali fulani kwa muda
 4. mbuzi :
  1. mnyama anayefugwa kama ng'ombe
  2. chombo cha kukunia nazi
 5. mlango :
  1. ukoo au watu wenye asili smoja
  2. sehemu ya kuingia kwenye nyumba
  3. kitu kinachotumika kifunga nyumba
 6. fua :
  1. unda vyombo/vifaa mbalimbali kwa kupiga chuma
  2. osha nguo
 7. vua :
  1. toa nguo kutoka mwilini
  2. toa samaki kwenye maji
 8. kiboko :
  1. mnyama mkubwa wa baharini
  2. silaha inayotumika kwa kuchapa au kupiga
 9. tembo :
  1. aina ya ndovu
  2. aina ya pombe

Visawe

Maneno tofauti yenye maana sawa.
 1. msichana au banati : ⇒ kijana wa jinsia ya kike
 2. mvulana au ghulamu : ⇒ kijana wa jinsia ya kiume
 3. huzuni au majonzi : ⇒ hali ya kilio na huruma
 4. mazishi au matanga : ⇒ shughuli za kumzika marehemu
 5. wakati au mwia : ⇒ wakati au muda
 6. mtu au mja : ⇒ mnyama atembeaye kwa miguu miwili mwenye uwezo wa kuongea na kufikiri kimantiki
 7. barua au waraka : ⇒ kartasi inayoandikwa na kutumwa ili kuwasilisha ujumbe fulani
 8. siri au faragha : ⇒ jambo lisilopaswa kujulikana na mtu mwengine
 9. macho au maninga : ⇒ sehemu za mwili zinazotumika kuangalia na kuona
 10. mwangaza au nuru : ⇒ miyale inayowezesha watu kuona vitu
 11. Mungu au Mola au Rabana au Jalali au Rabuka : ⇒ Majina ya Mwenyezi Mungu

15 Comments


Shukuru Misozi - May 10, 2013 @ 4:06pm

Naomba ufafanuzi, katika vitate 'fahali au ndume' limetumika kumaanisha ng'ombe dume lakini katika visawe 'fahali au ndume' imetumika kumaanisha anayesoma, anayefundishwa. Hapo sielewi maana hiyo iliyotolewa.

Master You - May 14, 2013 @ 3:14pm

Thanks for helping me i'm real appreciating for U Galfkosoft
Paneli la Kiswahili

Mwalimu Ouko - Jun 04, 2013 @ 8:48pm

jinsi ninavyofahamu neno fahali huenda ikamaanisha ng'ombe dume au shujaa.Asanteni mabingwa.

Mbuva - Jun 09, 2013 @ 5:35pm

fahali ni ng'ombe dume hii ya kama mwalimu na mwanafunzi inanitatiza tafadhali naomba ufafanuzi

ERIC OLESO - Jun 11, 2013 @ 6:47am

Asante sana

Donald Barasa - Jun 18, 2013 @ 7:58am

Naomba mnisaidie maana ya sauti ghuna na mifano

azuri - Aug 21, 2013 @ 4:19pm

Naomba nifahamishwe maana ya maneno yafutayo.Kikembe;Kidue;Kitungule;kibebe na Kichengo.Ahsanteni kwa kazi nzuri muifanyayo

Omondi lwero - Oct 07, 2013 @ 1:43pm

Naomba unianishie matatizo ya kimatamshi katika kamusi vitate

joyce - Oct 16, 2013 @ 11:27am

Naomba visawe vya nambari zifuatazo, moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, nane, tisa, kumi, kumi na moja

Mhuville, H. - Dec 24, 2013 @ 4:46am

mvulana ambaye bado hajabalehe anaitwaje?

K. DANIEL - Oct 22, 2014 @ 11:23am

nini kisawe cha neno asali

MM.SHIBLI - Dec 09, 2014 @ 1:52pm

JOYCE, mimi nakupa sufuri au nungi

MUNEZERO Aimé - Apr 22, 2015 @ 11:27am

shukrani kwenu kabisa. Nini kinyume ya
1. jogoo
2. shemeji

GIDEON MUTEMBEI NKOROI - 5 weeks ago

Asante kwa kazi kuntu

Miriti smog - 2 weeks ago

Nawasalimu nyote. pressure lamp inaitwaje kwa kiswahili ?

Login to CommentSauti Tamu
St. Paul's Students Choir is launching an app through which customers can order, pay and receive their music through their smart phones or choir website . You can get lyrics, mp3s and videos, for all our albums. Try the app Sauti Tamu mobile app.

A new approach to spread the gospel to all nations. The app also supports automated music sales for M-Pesa (Kenya and Tanzania).

Try it today! Perhaps this is what you/your choir has been looking for!