Virai na Vishazi


VIRAI NA VISHAZI
Kitengo Lugha
NAVIGATION
Next Aina za Sentensi
Prev Uchanganuzi wa Sentensi

Sentensi huwa na vifungu mbalimbali. Baadhi ya vifungu hivi ni vishazi na virai.

Virai (phrase)

Kirai ni fungu la maneno lisilokuwa na kitenzi.Phrase

Kuna aina nne za virai:

Kirai Nomino:

Kirai Nomino ni fungu la maneno katika sentensi lenye nomino (Kikundi Nomino/Kiima)
 1. Redio na runinga hutumika kutupasha habari.
 2. Bintiye Mchungaji Boriti anapenda kuwasaidia watu.
 3. Miembe mirefu itakatwa.

Kirai Kiwakilishi

Kirai Kiwakilishi ni fungu la maneno linalowakilisha nomino katika sentensi
 1. Zenyewe zimekwishaharibika.
 2. Watakaovumilia hadi siku ya mwisho wataokolewa
 3. Yeye alijitumbukiza majini na kufariki papo hapo.

Kirai Kivumishi

Kirai Kivumishi ni fungu la maneno katika sentensi linalotupa habari zaidi kuhusu nomino.
 1. Matokeotuliyokuwa tukiyasubiri yametangazwa.
 2. Duka zenye bei nafuu zimefungwa.
 3. Msichana mrembo kama malaika ameolewa.

Kirai Kielezi

Kirai Kielezi ni fungu la maneno linaloelezea zaidi kuhusu kitenzi au kivumishi.
 1. Walevi wana mazoea ya kupayuka ovyo ovyo.
 2. Viumbe vyote vyenye uhai vinamshangilia kwa furaha milele na milele.
 3. Kwaya ya Chuo Kikuu cha Nairobi huimba kwa sauti za kimalaika

Vishazi (clause)

Kishazi ni sehemu ya sentensi yenye kitenzi. Kuna aina mbili za virai:

Kishazi Huru (Independent Clause)

Kishazi Huru huwa na maana kamili na kinaweza kujisimamia chenyewe kama sentensi.
 1. Amina ameanza kuimba baada ya kumaliza kusali.
 2. Watakaopatikana wakichekacheka ovyoovyo, watang'olewa meno.
 3. Nitakupatia nusu ya ufalme wangu, iwapo utanipigia magoti.

Kishazi Tegemezi (Dependent Clause)

Kisha Tegemezi huhitaji kuunganishwa na kishazi kingine ili kuleta maana iliyokusudiwa. Aghalabu huwa na kirejeshi k.v amba-, -enye n.k
 1. Amina ameanza kuimba baada ya kumaliza kusali.
 2. Watakaopatikana wakichekacheka ovyoovyo, watang'olewa meno.
 3. Nitakupatia nusu ya ufalme wangu, iwapo utanipigia magoti.

40 Comments


Burhoney mponda - May 12, 2013 @ 7:25am

MImi ni mwanafunzi wa kidato cha sita nchini tanzania ninamkanganyiko juu ya aina za virai kuna baadhi ya vitabu huandika kuna kirai kitenzi na vingine hupinga hudai ikiwa kuna kirai tenzi kishazi cha nini nashindwa kujua ukweli halisi nisaidieni juu ya hilo

Burhoney mponda - May 12, 2013 @ 7:27am

pia kwa mapendekezo zaidi mngechambua miundo ya virai na vishazi asanteni sana kwa mchango wenu katika kuikuza lugha yetu ya kiswahili

MURUNGI NICHOLAS - May 23, 2013 @ 8:31am

kirai ni kipashio cha kiimuundo ambacho hakichukui muundo wa kiima na kiarifa.Tunaajua kwamba kuna kirai kitenzi.Je ni sahihi kusema kuwa kirai huwa hakina kitenzi?Kwangu mie haifai.

kipingi salmon - Jun 06, 2013 @ 3:39am

kwa mtazamo wangu kuna aina tano za virai na sio nne kama baadhi ya wadau wanavyosema.Aina hizo ni 1.kirai nomino, 2.kirai kitenzi, 3.kirai kivumishi, 4.kirai kielezi, 5.kirai kihusishi.kwa maelezo zaidi rejea DAFINA YA LUGHA sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu.

Idd Mikoko - Jun 07, 2013 @ 5:31am

mnapo weka hizi pegi mue mnaweka kwa undani zaidi coz tunotumia ni wengi mpaka wanafunzi wa vyuo pia

Idd Mikoko - Jun 07, 2013 @ 5:35am

naomba muainisho wa vishazi kwa njia ya kimaana na kimofolojia au kimaumbo

SOLO YEGON - Jun 17, 2013 @ 1:06pm

mnaposema hamna virai vitenzi mnanikanganya naomba mfafanue zaidi

Jay Nassir - Jun 18, 2013 @ 12:59pm

Ningependa kuwashukuru sana! Tuendelee kutukuza kiswahili!

joseph muriithi mugo - Sep 09, 2013 @ 10:28am

Naomba kidogo mrejelee suala la virai hasa kirai kitenzi. Kwa mujibu wa Kiswahili Kitukuzwe kid.3 kilichochapichwa na Kenya Literature Bureau (silabasi mpya) uk. 137-138, wadau hawa wana maoni kuwa mna kirai kitenzi. Suala hili kidogo lakanganya. Naomba ufafanuzi. Asante.

Manza Bay - Oct 08, 2013 @ 11:36pm

jamani naomba niwasaidie kidogo mana mimi ni mtaalamu wa hili somo, tunasoma aina za virai tunasoma kuwa ni 5 ambazo nia kirai nomino, kirai kiwakilishi, kirai kivumishi, kirai kitenzi na kirai kielezi ila kumbuka kuwa kirai hakina muundo wa KIIMA na KIARIFU, hivyo basi unaposema kirai kitenzi haimainishi kuwa unaweza kupata kiima na kiarifu labda ni wawekee sifa za virai kisha mtaelewa vizuri
SIFA ZA KIRAI
1.Kirai hakina muundo wa KIIMA - KIARIFU
2.Kirai ni tungo - yaani ni aina moja wapo katika aina 4 za tungo ambazo ni tungo neno, kirai, kishazi na sentensi
3.Kirai ni kikubwa kuliko tungo neno na ni kidogo kuliko tungo kishazi yaani tungo neno huundwa na silabi (muundo wa neno) lakini tungo kirai huundwa na neno au kifungu cha maneno
4.Kirai hakiwezi kutoa taarifa kamili kinaposimama peke yake labda kama ni jibu, yaani katika aina 5 za virai nilizozitaja hakuna ambayo inaweza kutoa taarifa kamili inaposimama peke yake labda kama ni jibu la swali aliloulizwa mtu kwa mafano yule anafanya nini ? JIBU ni "analima" neno analima ni jibu na ni kirai kitenzi lakini likisimama peke yake huwezi kupata taarifa kamili
5. kirai kinaweza kupatikana au kujitokeza upande wowote wa sentensi yaani KIIMA au KIARIFU
kwa maelezo zaidi nitafute kupitia mmohamedi @yahoo.com

yahya juma - Oct 13, 2013 @ 12:17am

Kiswahili kwanza!!

kiptoo langat - Oct 17, 2013 @ 1:21am

zadakta

Kibe - Oct 22, 2013 @ 3:29am

Swala la Virai ni tata yaonekana hivyo. Kiswahili Kitukuzwe Kidato cha 2 na Kiswahili Kitukuzwe Kidato cha 3: ufafanuzi tofauti kabisa; Gafkosoft maelezo tofauti. Liwe jukumu la wasomi wote kutambua virai ni nini hasa.

Juma waziri - Feb 20, 2014 @ 3:18pm

Maana ya kirai bado haijatolewa hapa

Njeri Kamau - Feb 23, 2014 @ 6:16am


Njeri Kamau - Feb 23, 2014 @ 6:20am

Swala hili la virai lastahili kuvaliwa njuga na wasomi wa Kiswahili kwani tunawakanganya wanafunzi kwa vitabu ambavyo vina maelezo tofauti. Twastahili tuwe na msimamo mmoja tena thabiti kuhusu swala zima la virai.

Festus - Mar 23, 2014 @ 1:40pm

kongole

PAUL KISSIMA - Apr 13, 2014 @ 3:24am

Tusichanganywe na wandishi wa vitabu wapo kibishara na si kuelimisha jamii.
Tuelewe maana inatosha kutoa tofauti ya kirai na kishazi
Kirai ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi na hakina muundo wa kiima na kiarifu mf kaka, nyau ,waliotembea
Kirai ktenzi kimechukuliwa kwa muktadha wa fungu la maneno ambalo linaweza kusimama pasipo kuwa na kiima na kiarifu bila kuangalia msingi wa sifa za kitenzi katika kiswahili
NB:tukumbuke vitenzi visaidiz havina muundo wa kiima na kiarifu
Kishazi tunasimamia msingi wa kitenzi na sifa zake katika kiswahili

Saulo Simon Mrutu - May 05, 2014 @ 8:27am

Kirai kinaweza kuelezewa kama kifungu cha maneno ambacho hutoa taarifa fulani. Ila hakina muundo wa kiima na kiarifu.

marypurity@uandishi mwafaka wa insha - May 13, 2014 @ 2:13am

kama kirai hakina maana kitwezaje kubeba kitenzi na kitenzi huonyesha jambo litokealo kwa nomino hivyo kutoa maana halisi ya linaloelezewa ? kitenzi kikitolewa huwa kiarifa na kiima kipo kwani kiima huweza kuwa kiwakilishi . wenzangu tusikanganyike!!

marypurity@uandishi mwafaka wa insha - May 13, 2014 @ 2:14am

tusaidiane katika mengi.

Mwalimu Mussa Shekinyashi - May 27, 2014 @ 4:15am

Mimi nataka jaribu kutoa maana tofauti ya kirai. Kwa kadri ninavyoendelea kufundisha sarufi ya kiswahili naona kuna upungufu wa kiasi kikubwa katika fasili ya dhana kirai hasa kwa wanafunzi wa kidato cha tatu na nne nchini Tanzania. Fasili kuu tunayoitumia ni ile ya kusema "Kirai ni tungo isiyo na muundo wa kiima na kiarifu".
Kwa upande wangu, Kirai ni tungo inayojumuisha neno moja au kikundi cha maneno chenye neno kuu ambacho hufanya kazi kama neno moja kwa ujumla wake katika sentensi.
Hii ina maana sawa na kusema "phrase is a group of words having a head word that functions as whole in a sentence".
Maana hii haitakuwa na utata kwa sababu haijataja dhana kitenzi kuwepo au kutokuwepo kwake ili kuifafanua dhana kirai.
Hivyo, mwanafunzi anaweza kufafanuliwa zaidi kuwa aina za virai hutegemea maneno yanayounda kirai hicho mapoja na uhusiano wake na neno kuu.
Mifano;
Ally-kirai Nomino
Ally na Zuena-Kirai Nomino
Msichana aliyevaaa viatu virefu vyeusi vyembaba -Kirai Nomino
Anakimbia -Kirai Kitenzi
Alikuwa anakimbia -Kirai Kitenzi
Vifupi vinene vyeupe -Kirai Kivumishi
N.k
Hapo nahisi afadhari mwanafunzi anweza kupata wazo juu ya dhana anayojifunza

FRIDAY JULIUS MUHABWA - Jul 04, 2014 @ 2:05am

Asante sana wataalamu na walimu wa kiswahili!
Nataka kujua mengi juu ya virai na vishazi

baldwin mwarigha - Jul 07, 2014 @ 5:15am

kuna vitabu ambavyo husema hakuna kirai kitenzi na pia baadhi ya mitandao, nisaidieni tafadhali, je kirai kitenzi kipo ama hakipo?

Okoth kevin owiti - Jul 09, 2014 @ 12:16pm

Kirai hujijenga katika msingi wa neno kuu, kwamba katika Kirai Nomino, neno kuu ni nomino. Itakuwa vigumu kuzingatia mfano huu:WATAKAOVUMILIA HADI SIKU YA MWISHO, wataokolewa. Kwa sababu matumizi ya kirejeshi 'O' yanasababisha utegemezi. Muundo wake aidha ni wa KIIMA na KIARIFU.

makata - Aug 15, 2014 @ 1:19am

nimesaidika sana

kubai haron mutuma - Aug 27, 2014 @ 4:39am

nimesaindika kwa kuongeza yale ninanayojua ,kwa hivyo ningependa mnisaindie kujibu hili swali :ukitumia kigezo cha semantiki na uku ukitolea mifano ainisha ngeli za kiswahili

david moranga - Dec 19, 2014 @ 2:39am

ahsanteni Kwa Msaada wenu,mmenijenga kielimu na kunielimisha hata zaidi.Hebu kiswahili kitukuzwe hata zaidi.

Rashid mbwana - Jan 07, 2015 @ 11:34pm

Nikiwa shuleni niliona haya mambo kua magumu sana
Sikujua kuhusu gafkosoft

Miss OliviaMcOdero - Jan 09, 2015 @ 9:16am

bado sijaelewa maana ya kirai

mwalimu manwa - Mar 18, 2015 @ 8:07am

langu ni swali tu,ni vipi tukawa na kirai kiwakilishi ilhali katika ufafanuzi Wa kirai nomino ni kuwa ni fungu lililo na nomino na viwakilishi vyake.. pili tunaporejelea kionyeshi cha kirai vitabu vingine hutumia herufi R\' je no sawa?

Damaris Githinji - Mar 30, 2015 @ 7:44am

Kirai ni neno au fungu la maneno linaloongozwa na neno moja kuu au ni neno au fungu la maneno linalodokeza maana lakini si kamilifu. Kuna aina nne za virai, Kirai nomino- neno kuu ni nomino, Kirai kitenzi- neno kuu ni kitenzi, kirai elezi- kielezi na kirai kihusishi neno kuu ni kihusishi. Kirai kitenzi kipo kwani maana ya kimuundo ya kirai ni kikundi. Viwakilishi viko chini ya virai nomino.

daniel mandila - Mar 30, 2015 @ 3:49pm

Heko na kongole kwa ufanuzi wa virai hasa mw. Monza au Mohammed. Vitabu viko biashara kutupotosha tu

Damaris Githinji - Apr 10, 2015 @ 5:12pm

Naomba kujikosoa kuhusu virai. Aina ni tano bali si nne kama nilivyodokeza hapo awali. Kirai kivumishi kiliachwa kimakosa.

Amirinho - Apr 22, 2015 @ 12:51pm

Ahsanteni

paul - May 26, 2015 @ 4:27pm

SAFI SANA KAKA DAMARIS KWA UKOMAVU KITAALUMA

Des Kilalu - Jun 19, 2015 @ 1:46pm

kazi nzuri

John mutua - Jun 21, 2015 @ 5:04am

Ningependa kupata uchambuzi wa riwaya kidagaa kimemwozea na ken walibora

Samson Yongo - Jun 23, 2015 @ 1:45pm

Anwani ni jazanda.wataka 2anze wapi?

JACKSON MWAMBAJI - Jul 16, 2015 @ 1:14am

mimi ni mwanafunzi wa kidato cha nne (kenya).nmekua na mkanganyiko upande wa virai. kuna baadhi ya vitabu haviweki wazi kuweko kwa kirai kitenzi. vyengine vina eleza kuweko kwa aina mbili pekee za virai ambazo ni kirai nomino na kirai kitenzi. maelezo haya yananikanganya naombe mnisaidie

Login to CommentSauti Tamu
St. Paul's Students Choir is launching an app through which customers can order, pay and receive their music through their smart phones or choir website . You can get lyrics, mp3s and videos, for all our albums. Try the app Sauti Tamu mobile app.

A new approach to spread the gospel to all nations. The app also supports automated music sales for M-Pesa (Kenya and Tanzania).

Try it today! Perhaps this is what you/your choir has been looking for!