Uchanganuzi wa Sentensi


UCHANGANUZI WA SENTENSI
Kitengo Lugha
NAVIGATION
Next Virai na Vishazi
Prev Muundo wa Sentensi

Kuchanganua sentensi ni kugawa sentensi kulingana na makundi ya maneno na aina ya maneno.

Kuna njia tatu za kuchanganua sentensi:
 1. matawi
 2. jedwali
 3. mishale

Mifano

Kuchanganua Sentensi Sahili

1. Nimefika.

 1. Matawi
  Changanua kwa njia ya Matawi
 2. Jedwali
  S
  KT
  T
  Nimefika
 3. Mishale

  S → KT

  KT → T

  T → Nimefika

2. Jiwe Limeanguka.

 1. Matawi
  Changanua kwa njia ya Matawi
 2. Jedwali
  S
  KN KT
  N T
  Jiwe limeanguka
 3. Mishale

  S → KN + KT

  KN → N

  N → Jiwe

  KT → T

  T → limeanguka

3. Mvua nyingi ilinyesha jana usiku.

 1. Matawi
  Changanua kwa njia ya Matawi
 2. Jedwali
  S
  KN KT
  N V T KE
  T E E
  Mvua nyingi ilinyesha jana usiku
 3. Mishale

  S → KN + KT

  KN → N + V

  N → Mvua

  V → nyingi

  KT → T + KE

  T → ilinyesha

  KE → E1 + E2

  E1 → jana

  E2 → usiku

Kuchanganua Sentensi Ambatano

1. Barua ilitumwa lakini haikumfikia Shakila.

 1. Matawi
  Changanua kwa njia ya Matawi
 2. Jedwali
  S
  S1 U S2
  KN1 KT1 U KT2 KN2
  N1 T1 U T2 N2
  Barua ilitumwa lakini haikumfikia Shakila
 3. Mishale

  S → S1 + U + S2

  S1 → KN1 + KT1

  KN1 → N1

  N1 → Barua

  KT1 → T1

  T1 → ilitumwa

  U → lakini

  S2 → KT2 + KN2

  KT2 → T2

  T2 → haikumfikia

  KN2 → N2

  N2 → Shakila

2. Mwalimu alikunja shati lake na kuwachapa wanafunzi kwa kiboko.

 1. Matawi
  Changanua kwa njia ya Matawi
 2. Jedwali
  S
  S1 U S2
  KN KT U KT KN
  N T KN U T KN KE
  N T N V U T N U N
  mwalimu alikunja shati lake na kuwachapa wanafunzi kwa kiboko
 3. Mishale
  S → S1 + U + S2

  S1 → KN1 + KT1

  KN1 → N

  N → mwalimu

  KT1 → T + KN2

  T → alikunja

  KN2 → N + V

  N → shati

  V → lake

  U → na

  S2 → KT2 + KN3 + KE

  KT2 → T

  T → kuwachapa

  KN3 → N

  N → wanafunzi

  KE → U + N

  U → kwa

  N → kiboko

Kuchanganua Sentensi Changamano

1. Wote waliokufa watafufuka

 1. Matawi
  Changanua kwa njia ya Matawi
 2. Jedwali
  S
  KN KT
  W s T
  Wote waliokufa watafufuka
 3. Mishale
  S → KN + KT

  KN → N + s

  W → wote

  s → waliokufa

  KT → T

  T → watafufuka

2. Wanafunzi ambao hawatasoma vizuri wataanguka mtihani

 1. Matawi
  Changanua kwa njia ya Matawi
 2. Jedwali
  S
  KN KT
  N s T N
  N V KT T N
  N V T E T N
  Wanafunzi ambao hawatasoma vizuri wataanguka mtihani
 3. Mishale
  S → KN + KT

  KN → N + s

  N → wanafunzi

  s → V + T + E

  V → ambao

  E → hawatasoma

  KT → T + N

  T → wataanguka

  E → mtihani


18 Comments


Elijah Mwaniki Njue - Apr 05 2013, 3:30am

Katika uchanganuzi wa sentensi kuna dosari kidogo.

MAKULA SANGUDI - Apr 11 2013, 7:22am

naomba mtoe sifa bainifu za aina za sentensi kabla hamja changanua pia ikiwezekana toeni marejeo. kazi ni nzuri

RICHARD MHAGAMA - Apr 25 2013, 12:03pm

naomba mtoe kanuni za uchanganuzi ,pia ikiwezekana toeni sifa bainifu kwa kila aina ya neno.

steve enoka odera bunde - Jun 11 2013, 2:51am

naomba kujua kama katika uchanganuzi wenu, kishazi pia kinafaa kuchanganuliwa zaidi?

mutuma peter - Jun 26 2013, 4:01am

naomba mnifafanunulie kama inafaa kuchanganua sentensi kwa njia ya kutumia mabano.kwa sababu kuna baadhi ya vitabu vinachanganua hivyo.mimi ni mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha egerton nchini kenya.asanteni.

Samuel M.Ng'ang'a - Jul 17 2013, 2:19am

Katika uchanganuzi wa sentensi changamano kishazi tegemezi huonyeshwa kama fungu moja.Katika uchanganuzi wa sentensi yoyote kama kundi nomino halipo linaonyeshwa lakini unaandika kapa katika sehemu tunayoonyesha aina za maneno.

ELIEWAHA MSANGI - Sep 18 2013, 8:40am

Hebu tujuze hivyo vi-------s-------katika sentensi changamano ndio vinyama gani? Pia hukueleza juu ya Njia ya maelezo na njia ya mabano, tufunze

pius kaburu mugambi - Sep 30 2013, 7:34am

naomba kujua maana ya KN,S ,T,N,E,KT,V

Tanzania Nchi Yetu Sote - Oct 23 2013, 12:39am

Baadhi ya vitabu kama KISWAHILI KIDATO CHA TANO NA SITA toleo la kwanza (2012) OXFORD wamechanganua sentensi kwa kutumia mikabala ya kimapokeo (kikazi) wakitumia Kiima (K) na Kiarifu (A) pamoja na mkabala wa Kimuundo KN na KT sasa je ucanguzi upi ufuatwe?

KAKONJAGILE EDSON - Feb 06 2014, 5:54am

Majibu kwa bwana pius kaburu, KN-kundi nomino, S-sentensi, T-kitenzi, N-nomimo, E-kielezi, KT-kundi tenzi na V-vumishi

MTOTO MDOGO - 7 weeks ago


MTOTO MDOGO - 7 weeks ago

HIYO 'S' KWENYE KUNDI NOMINO INA MAANA GANI?

Njeri Kamau - 7 weeks ago

Nafikiri ile s ina maana ya kishazi tegemezi. Ahsanteni mabingwa kwa uchanganuzi huo mzuri.

Steven william - 6 weeks ago


Onyiego Geofrey - 6 weeks ago

Hongera mabingwa kwa kazi nzuri.

Onyiego Geofrey - 6 weeks ago

S katika uchanganuzi huu ina maana ya sentensi

odiga paul james - 5 weeks ago

Asanteni Sana wanapaneli

alicia kahuthu - 4 weeks ago

Login to Comment