Ngeli za Kiswahili


NGELI ZA KISWAHILI
Kitengo Sarufi
NAVIGATION
Next Ukubwa na Udogo
Prev NGE na NGALI

Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Katika mfumo wa kisasa (na unaokubalika), ngeli huundwa kwa kuunganisha viambishi viwakilishi vya nomino.

Kwa mfano, neno kitabu. Tunasema, "Kitabu kimepotea - Vitabu vimepotea."

Kwa kuunganisha kiambishi "KI"(umoja) na VI(wingi), tunapata ngeli ya KI-VI. Ni muhimu kusisitiza kwamba tunazingatia viambishi, wala si silabi ya kwanza.

Hivyo basi, maneno yasioyoanza kwa KI-VI kama vile chama -vyama yatakuwa katika ngeli ya KI-VI kwa kuwa yanachukua kiambishi KI => (Chama kimevunjwa - Vyama vimevunjwa.) Vivyo hivyo, kunayo majina yanayoanza kwa KI-VI yasiyokuwa katika ngeli ya KI-VI maadam yanachukua viambishi tofauti. k.v: kijana => A-WA (kijana amefika- vijana wamefika).

Tumekuandalia majedwali matatu kukupa mukhtasari wa ngeli zote za Kiswahili na jinsi baadhi ya maneno/viambishi vinavyobadilika kutoka ngeli moja hadi nyingine.


a) Jedwali la kwanza linakupatia ngeli, maelezo yake, na mifano ya majina:

NGELI MAELEZO MIFANO
A-WA

Hii ni ngeli ya majina ya viumbe wenye uhai k.v watu, wanyama, ndege, wadudu, miungu, malaika n.k Majina mengi katika ngeli ya A-WA huanza kwa sauti M- kwa umoja na sauti WA- kwa wingi. Hata hivyo baadhi ya majina huchukua miundo tofauti.

mtu - watu
KI-VI

Ni ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo. k.v kitoto.

kitu - vitu
LI-YA

Hujumuisha majina ya vitu visivyo hai pamoja na yale ya ukubwa k.v jitu. Majina yake huchukua miundo mbalimbali. Baadhi yake huchukua muundo wa JI-MA (jicho-macho), lakini yanaweza kuanza kwa herufi yoyote. Kwa wingi, majina haya huanza kwa MA- au ME-.

jani - majani
U-I

Huwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI(wingi).

mti - miti
U-ZI

Hurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/' k.v ukuta-kuta. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. k.v ufa - nyufa

ukuta - kuta
I-ZI

Hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (Wingi). Mengi yake huanza kwa sauti /u/, /ng/, /ny/, /mb/, n.k

nyumba - nyumba
U-YA

Ni majina machache mno yanayochukua kiambishi U(umoja) na YA(wingi).

uyoga - mayoga
YA-YA

Hii ni ngeli ya vitu visivyoweza kuhesabika (nomino za wingi). Hayana umoja. Mengi ya majina haya huanza kwa MA- lakini yanaweza kuchukua muundo wowote.

maji
I-I

Ni ngeli ya majina ya wingi ambayo huchukua kiambishi I- kwa umoja na pia kwa wingi. Majina haya hayana muundo maalum.

sukari
U-U

Majina ya nomino za wingi yanayoanza kwa sauti /u/ au /m/. Hayana wingi.

unga
PA-PA

Ni ngeli ya mahali/pahali - maalum.

mahali
KU-KU

Ngeli ya mahali - kwa ujumla. Aidha, hujumuisha nomino za kitenzi-jina

uwanjani
MU-MU

Ngeli ya mahali - ndani.

shimonib) Jedwali la pili linaangazia jinsi ngeli mbalimbali zinavyotumia "a-nganifu", viashiria na viashiria visisitizi.

NGELI A- UNGANIFU VIASHIRIA VIASHIRIA VISISITIZI
KARIBU MBALI KIDOGO MBALI KARIBU MBALI KIDOGO MBALI
A-WA wa
wa
huyu
hawa
huyo
hao
yule
wale
yuyu huyu
wawa hawa
yuyo huyo
ao hao
yule yule
wale wale
KI-VI cha
vya
hiki
hivi
hicho
hivyo
kile
vile
kiki hiki
vivi hivi
kicho hicho
vivyo hivyo
kile kile
vile vile
LI-YA la
ya
hili
haya
hilo
hayo
lile
yale
lili hili
yaya haya
lilo hilo
yayo hayo
lile lile
yale yale
U-I wa
ya
huu
hii
huo
hiyo
ule
ile
uu huu
ii hii
uo huo
iyo hiyo
ule ule
ile ile
U-ZI wa
za
huu
hizi
huo
hizo
ule
zile
uu huu
zizi hizi
uo huo
zizo hizo
ule ule
zile zile
I-ZI ya
za
hii
hizi
hiyo
hizo
ile
zile
ii hii
zizi hizi
iyo hiyo
zizo hizo
ile ile
zile zile
U-YA wa
ya
huu
haya
huo
hayo
ule
yale
uu huu
yaya haya
uo huo
yayo hayo
ule ule
yale yale
YA-YA ya haya hayo yale yaya haya yayo hayo yale yale
I-I ya hii hiyo ile ii hii iyo hiyo ile ile
U-U wa huu huo ule uu huu uo huo ule ule
PA-PA pa hapa hapo pale papa hapa papo hapo pale pale
KU-KU kwa huku huko kule kuku huku kuko huko kule kule
MU-MU mwa humu humo mle mumu humu mumo humo mle mlec) Jedwali la pili linaangazia virejeshi(-o, amba-, -enye, -enyewe), ote, o-ote, ingi, ingine n.k kulingana na ngeli mbalimbali.

NGELI KIREJESHI O-REJESHI (AMBA-) ENYE ENYEWE OTE O-OTE INGI INGINE
A-WA ye
o
ambaye
ambao
mwenye
wenye
mwenyewe
wenyewe
wote
wote
yeyote
wowote
mwingi
wengi
mwengine
wengine
KI-VI cho
vyo
ambacho
ambavyo
chenye
vyenye
chenyewe
vyenyewe
chote
vyote
chochote
vyovyote
kingi
vingi
kingine
vingine
LI-YA lo
yo
ambalo
ambayo
lenye
yenye
lenyewe
yenyewe
lote
yote
lolote
yoyote
jingi
mengi
jingine
mengine
U-I o
yo
ambao
ambayo
wenye
yenye
wenyewe
yenyewe
wote
yote
wowote
yoyote
mwingi
mingi
mwingine
mingine
U-ZI o
zo
ambao
ambazo
wenye
zenye
wenyewe
zenyewe
wote
zote
wowote
zozote
mwingi
nyingi
mwingine
nyingine
I-ZI yo
zo
ambayo
ambazo
yenye
zenye
yenyewe
zenyewe
yote
zote
yoyote
zozote
nyingi
nyingi
nyingine
nyingine
U-YA o
yo
ambao
ambayo
wenye
yenye
wenyewe
yenyewe
wote
yote
wowote
yoyote
mwingi
mengi
mwingine
mengine
YA-YA yo ambayo yenye yenyewe yote yoyote mengi mengine
I-I yo ambayo yenye yenyewe yote yoyote nyingi nyingine
U-U o ambao wenye wenyewe wote wowote mwingi mwingine
PA-PA po ambapo penye penyewe pote popote pengine
KU-KU ko ambako kwenye kwenyewe kote kokote kwingi kwengine
MU-MU mo ambamo mwenye mwenyewe mote momote mengine
62 Comments


lokadabui - Jan 23, 2013 @ 8:07pm

maiti liko katika ngeli ipi? shukran

Guest Mgeni - Mar 03, 2013 @ 11:24pm

Maiti kaka iko katika ngeli ya I-ZI

Guest Mgeni - Mar 12, 2013 @ 5:11am

Je PANA ngeli ya vi? Na mfano wake ni upi?

-mwambura-

victor - Mar 28, 2013 @ 8:24am

majina gani hayapo kwenye ngeli za upatanisho wa kisarufi? na kwanini?

Mwalimu Geoffrey Mosigisi - Mar 29, 2013 @ 4:38pm

Je, jina jua hupatikana katika ngeli gani?

Administrator - Mar 30, 2013 @ 11:29am

Neno 'Jua' liko katika ngeli ya LI-YA. Kungalikuwa na jua jingine duniani au sayari nyingine, tungalisema 'jua - majua'; 'jua limewaka - majua yamewaka'

JEREMIA MWANZA - Apr 08, 2013 @ 12:24pm

Je,ngeli "UASI" ipo ngeli ipi?

JEREMIA MWANZA - Apr 08, 2013 @ 12:27pm

Je, kuna nomino U-MA?

JEREMIA MWANZA - Apr 08, 2013 @ 12:27pm

Je, kuna nomino U-MA?

MAKULA SANGUDI - Apr 11, 2013 @ 7:23am

maziwa maji yako kwenye ngeli gani

JEREMIA MWANZA - Apr 14, 2013 @ 1:55am

Maji na maziwa ni ngeli ya 'YA-YA' Ambayo huwa ni ya majina ya vitu visivyohesabika vyenye kuanza na silabi MA..

Joseph mwachi - Apr 17, 2013 @ 8:29am

Je,uainishaji wa kimofolojia una manufaa gani kwa msomi wa kiswahili.

kelvin motuka - May 18, 2013 @ 4:41am

neno 'uyoga' liko katika ngeli gani?

Sanya marwa - May 26, 2013 @ 4:54am

Neno nyoya iko katika ngeli gan

felix sirere - Jun 07, 2013 @ 7:06am

maiti iko ngeli gani

kamau - Jun 30, 2013 @ 1:00pm

jina mvua liko katika ngeli gani?

jim nyarindo - Jul 03, 2013 @ 1:41pm

tofauti ipi iliyoko baina ya ngeli ya LI-YA na U-YA
maiti kwa maoni yangu liko ngeli ya A-WA

BRIMER OGINGA - Aug 14, 2013 @ 3:37am

neno maktaba liko katika ngeli gani?

Elikana Simiyu Wafula - Sep 03, 2013 @ 1:21am

Neno maiti liko katika ngeli ya A-WA hii ni kulingana na heshima na faiwati ya binadamu. Pia utapata marehemu ambaye bado ni maiti yuko katika ngeli ya A-WA

Bichwa, Saul - Sep 25, 2013 @ 1:15am

Mtoa mada, katika ngeli ya U-I umeenda chaka. Hebu chunguza maelezo yako hapa. "U-I
Huwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI(wingi)." Kwa hali halisi miti ni viumbe hai lakini siyo wanyama, wadudu wala ndege. Hivyo ulitakiwa useme vitu visivyo hai hai na viumbe walio hai(wasio wanyama, ndege wala wadudu). Hapo imekaa vizuri.
mti - miti

Erasmus Francis - Oct 13, 2013 @ 7:45am

Neno UASI lipo katika ngeli ya U-YA, kwani tunasema katika kiwsahili fasaha kuwa, Uasi umezuka - Maasi ya Yameibuka, hapa tunachokiangalia ni upatanisho wa kisarufi na wala si maumbo ya umoja na wingi katika nomino

Erasmus Francis - Oct 13, 2013 @ 7:49am

Nomino za U-MA ni pamoja na Ugonjwa - Magonjwa, Uovu -Maovu

ELIEWAHA MSANGI - Oct 18, 2013 @ 10:16am

WENZANGU-Unapotoa jibu sema unatumia mkabala gani Kimofolojia au Kisintaksia kwani kisintaksia neno ugonjwa liko katika ngeli ya U-YA Ugonjwa umeenea --Magonjwa yameenea.

ELIEWAHA MSANGI - Oct 18, 2013 @ 10:22am

Kwa mkabala wa kisintaksia neno maktaba linaingia ngeli ya 5 (I-ZI) maktaba imejengwa mjini Moshi----Maktaba zimejengwa mjini Moshi pia neno hili halina kiambishi cha wingi na umoja katika umbo lake.

ELIEWAHA MSANGI - Oct 18, 2013 @ 10:34am

Kisintaksia neno(( jua) liko katika ngeli ya Nomino zisizokuwa na na maumbo ya umoja na wingi. yaani ngeli ya 5
( I-ZI.) TUSAIDIANE SHULE WASHIKAJI PIA TUELEZANE VITABU TUNAVYOTUMIA

tanui samuel - May 27, 2014 @ 10:02pm

Neno pesa linapatikana katika ngeli gani? Pia andika sentensi ifuatayo kwa umojo. Pesa zangu zimepotea.

George Kodhek - May 28, 2014 @ 8:25am

Ngeli hizi pia ziongezwe- LI-LI k.m jua,giza, VI-VI k.m vita,virusi A-A k.m Mungu,

Kaka Imoli - May 28, 2014 @ 10:13am

Kazi sadakta sana,nomino:maktaba,maabara,mvua na matwana zinaorodheshwa katika ngeli zipi?

tanui samuel - May 28, 2014 @ 3:12pm

Tafadhali ningali nangoja jawabu la swali langu.

Antony mwangi - Jun 09, 2014 @ 2:50am

maiti iko katika ngeli ya a-wa,k.m maiti amezikwa-maiti wamezikwa.Tafadhali sipotoshe jamii nzima

baldwin mwarigha - Jul 07, 2014 @ 5:22am

naomba kujuzwa tafadhali... neno kiswahili liko katika ngeli gani?

NICOLE22 - Jul 09, 2014 @ 9:55am

@ Kelvin Motuka (Mei 18, 2013)jibu la swali lako liko kwenye jadwali la kwanza. Uyoga inapatikana katika ngeli ya U-YA

Mwalimu Mstaafu Isemek - Sep 20, 2014 @ 11:59am

Msaada wenu ni bora kwangu kwa wakati huu wa marudio ya kuwaandaa watahiniwa wa darasa la nane, tuweke Nomino MAITI katika ngeli gani?

FRIDAY JULIUS MUHABWA - Oct 06, 2014 @ 10:08pm

#mwalimugeofry masigisi mimi nafikili kwamba, jina jua liko katika ngeli ya ji-ma kwa sababu; katika (umoja) jua linawaka na(wingi) maua yana waka

MUSA MBONEA - Nov 23, 2014 @ 10:22am

wanafunzi wote tuhamie huku acheni kupoteza muda na mambo mengine ambayo hayana faida kwa masomo yenu

KIRIMI JACOB - Dec 04, 2014 @ 7:24am

Mfano wa nomino katika ngeli ya VI ni neno VITA
Ingawaje nomino hii haina wingi.
Natumai QUEST MGENI nimelijibu swali lako.

KIRIMI JACOB - Dec 04, 2014 @ 7:24am


Omondijunior - Dec 31, 2014 @ 12:14pm


Omondijunior - Dec 31, 2014 @ 12:16pm

Omera hii ni kazi shwari bila shari, shukran.......

kansigo chakupewa nkwabi - Jan 15, 2015 @ 2:04am

kazi nzuri sana ila kwa upande wangu nahisi aina za ngeli ninazozijua ni nane tu
na huwa natumia hii fomyula WA MI N KI MA U PA KU...

Adesheikh - Jan 30, 2015 @ 7:13am

Ni vizuri kuelimishana juu ya jambo fulani
Je,Neno hewa lipo katika ngeli gani?...........nashukuru.

Okeyo Brian - Feb 09, 2015 @ 1:34pm

Asenteni sana.je,kitenzi \'kazi\' ikokwa ngeli gani?

Mohammed - Feb 17, 2015 @ 10:47am

J͓̽e͓̽ n͓̽o͓̽ n͓̽o͓̽ i͓̽p͓̽o͓̽ k͓̽a͓̽t͓̽i͓̽k͓̽a͓̽ n͓̽g͓̽e͓̽l͓̽i͓̽ g͓̽a͓̽n͓̽i͓̽?

Craig Carlos - Mar 12, 2015 @ 12:08pm

Lugha ipo katika ngeli gani?

Jevin Boaz Oduor - Mar 16, 2015 @ 3:01am

#carlos
Lugha iko katika ngeli ya I-ZI kulingana na maoni yangu.

kariuki - Mar 22, 2015 @ 8:24am

Kutokana na heshima na hadhi za uhai wa binadam,neno MAITI, linapaswa kuainishwa katika ngeli ya A-WA.pia nikitazama mzozo katika sala la neno ,JUA, lipo katika ngeli ya LI-YA..japo wengi watasema kulingana na sababu za kisanyansi jua duniani ni moja tu na hivyo kwamba halipaswi kuwa na wingi.la hasha hapa tutazingatia viambishi vya ukubwa na utakapo weka neno hilo kwenye mizani utalipata kwenye ngeli ya LI-YA.

kariuki - Mar 22, 2015 @ 8:29am

naomba kusaidiwa kuelewa upungufu wa uainishaji wa ngeli kwa kutumia mtindo wa HESIBATI UKILINGANISHWA NA ULE WA KIMOFOLOJIA

noel munayi - Mar 28, 2015 @ 5:57am


noel munayi - Mar 28, 2015 @ 5:58am

naomba kuainishia ngeli za nomino Jonesboro

Edwin Musonye - Apr 13, 2015 @ 5:39am

Je, tofauti ya neno Tendo na neno Kitendo ni gani? Kwa sababu yanatenga kwa ngeli. Kwa mfano, wingi wa tendo ni matendo (ngeli ya LI-YA); nayo wingi wa kitendo ni vitendo (ngeli ya KI-VI)?

Mecklean Richard - May 22, 2015 @ 11:12am

kutokana na uzingatiaji wa upatanishi wa kisarufi katika uanishaji wa ngeli kwa kigezo cha kisintaksia inapelekea kuzingatia viambishi vya awali vya nomino katika setensi.hivo basi pale nomino inapopachikwa kiambajengo cha udogodishi,huadhiri pia ngeli ya nomino husika na kubadilika.mfano Nomino Mtoto ipo katika ngeli ya a-wa lakini ikidogodishwa na kua katoto. katoto itakua ngeli ya ki-vi kwakua ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo.hivyo basi hata Nomino Tendo inapodogodishwa itaingia katika ngeli ya ki-vi

Wafula wanjala victor - Jun 10, 2015 @ 3:39pm

Sadakta!

Aburo - Aug 23, 2015 @ 11:49pm

Nomino kiu iko katika ngeli ipi

mutua mwanzia - Aug 26, 2015 @ 7:35am

tunasema mali mengi ama mali nyingi wataalamu wa lugha?

Kilio Tafiti - 4 weeks ago

kiu ni nomino dhahania katika ngeli ya I kwa mujibu wa uainishaji wa ngeli kisintaksia kiu-kiu. Katika mfumo uu huu jina mali huainishwa katika ngeli ya Ya, maji-maji

kumAmazako - 3 weeks ago

kumamazenyu nyiniendeni mjifire doggie style.....shoga nyinyi kwanaza MUTUA MWANZIA,NA ABURO MSENGEE WEWE.nGOZI ZENU ZIMEKAUKA ZINAEZA TENGENEZA ATA KIATU NA MSHIPI..
HIII NAISULA FAGGOTS

kumAmazako - 3 weeks ago

WASENGEEEEE NAA WASENGEREE...

kumAmazako - 3 weeks ago

WASENGEEEEE NAA WASENGEREE...

kumAmazako - 3 weeks ago

WASENGEEEEE NAA WASENGEREE...

kumAmazako - 3 weeks ago

BY RONNIE KIBET ST CHRISTOPHERS SCHOOL....STUPID FOOOOLS NKTESSST KULENI MAVI NA MBOKI....MATITI YA NYOKA NYINYI!!!!!!!

kumAmazako - 3 weeks ago


kumAmazako - 3 weeks ago

KICHWA YA CICILIA THEO WEWE

Login to CommentSauti Tamu
St. Paul's Students Choir is launching an app through which customers can order, pay and receive their music through their smart phones or choir website . You can get lyrics, mp3s and videos, for all our albums. Try the app Sauti Tamu mobile app.

A new approach to spread the gospel to all nations. The app also supports automated music sales for M-Pesa (Kenya and Tanzania).

Try it today! Perhaps this is what you/your choir has been looking for!