SARUFI: Matumizi ya Lugha


Sarufi ni sheria, kanuni au taratibu zinazopaswa kufuatwa katika lugha fulani. Kila lugha huwa na kanuni zake. Katika sarufi tutazingatia sauti(utamkaji), aina ya maneno, upatanisho wa maneno kisarufi, muundo wa sentensi za Kiswahili na kadhalika.

Ufuatao ni mukhtasari wa baadhi ya yale tuliyokuandalia katika matumizi ya lugha. Fungua kila ukrasa ili kusoma mada kwa kina.

Vipashio vya Lugha

Vipashio vya lugha ni viungo mbalimbali vinavyowekwa pamoja katika mpangilio fulani kisarufi, kuunda lugha:

 1. Sauti
 2. Mofimu
 3. Neno
 4. Sentensi

Kwa kuzingatia vipashio hivi vya lugha, tumekuandalia vipengele vifuatavyo katika sarufi:

Aina za Maneno

 • Nomino - majina, aina za nomino, uundaji wa nomino kutoka kwa maneno mengine, wingi
 • Vitenzi - vitendo katika sentensi, aina za vitenzi, mnyambuliko wa vitenzi
 • Viwakilishi - maneno yanayowakilisha nomino; aina za viwakilishi
 • Vivumishi - aina za vivumishi k.v vivumishi vya sifa, n.k
 • Vielezi - vielezi halisi, vielezi vya namna n.k
 • Viunganishi - a-unganifu, kuonyesha tofauti, sababu, sehemu n.k
 • Vihisishi - maneno ya kuonyesha hisia k.v hasira, mshangao n.k
 • Vihusishi - uhusiano wa nomino na mazingira yake
 • Kinyume - kinyume cha maneno mbalimbali

Muundo wa Maneno

 • Sauti na Silabi - aina za sauti(konsonanti, vokali), silabi, matamshi
 • Shadda na Kiimbo - mkazo katika maneno, kiimbo(intonation)
 • Viambishi - maana na aina za viambishi, uainishaji
 • Mofimu - mofimo huru, mofimu tegemezi
 • Viungo - Matumizi ya viungo k.v KWA, KU, JI, MA, NI, NA n.k

Upatanisho wa Maneno

 • Ngeli - ngeli mbalimbali za Kiswahili k.v A-WA, KI-VI n.k
 • Umoja na Wingi - wingi/umoja wa nomino, sentensi n.k
 • Ukubwa na Udogo - onyesha ukubwa/udogo wa neno au sentensi
 • Nyakati na Hali - nyakati(uliopita, uliopo, ujao, n.k), NGE, NGALI,
 • Kukanusha - kukanusha sentensi katika hali na nyakati mbalimbali

SentensiSauti Tamu
St. Paul's Students Choir is launching an app through which customers can order, pay and receive their music through their smart phones or choir website . You can get lyrics, mp3s and videos, for all our albums. Try the app Sauti Tamu mobile app.

A new approach to spread the gospel to all nations. The app also supports automated music sales for M-Pesa (Kenya and Tanzania).

Try it today! Perhaps this is what you/your choir has been looking for!