Isimu Jamii


Isimu Jamii (social linguistcs) - ni tawi la isimu (elimu ya lugha) linalochunguza namna lugha inavyotumika katika jamii na uhusiano baina yake. Tawi hili huzingatia matumizi ya lugha katika mazingira tofauti; aina mbali mbali za lugha na mazingira yake; uhusiano kati ya lugha na utamaduni wa jamii inayoitumia.


Istilahi za Isimu Jamii

 1. Isimu (linguistics) - ni mtalaa ambao huchunguza, huchanganua na pia kuchambua na kufafanua lugha kama mfumo wa mawasiliano baina ya wanadamu.
 2. Lugha - ni chombo cha mawasiliano baina ya watu. Lugha huzingatia mpangilio maalum wa sauti, maneno na sentensi.
 3. Sajili - ni mukhtadha/rejista mbalimbali au mitindo maalum ya lugha katika mazingira/hali mbalimbali. Mifano ya sajili ni kama vile lugha ya hospitalini, shuleni, sajili ya dini, biashara, kisiasa, michezo,
 4. Fonolojia - ni tawi la sayansi ya isimu linaloshughulikia uchunguzi wa mfumo wa sauti katika lugha fulani, kwa mfano ugawanyaji wa irabu na konsonanti. Fonolojia hutumika kuunda alfabeti katika lugha fulani. Aghalabu kila lugha hutumia mfumo fulani wa sauti mahususi katika lugha hiyo pekee.
 5. Fonetiki - huchunguza sauti zinazotamkwa na binadamu bila kuzingatia lugha yoyote.
 6. Mofolojia - (au sarufi maumbo) ni tawi la isimu linalochunguza maneno ya lugha fulani, aina za maneno katika lugha, hasa upangaji wa mofimu mbalimbali zitumikazo kwa ajili ya kuunda maneno hayo. Kwa mfano, lugha ya Kiswahili hutumia mbinu kadhaa kuunda maneno kulingana na mpangilio wa mofimu. Kwa mfano, neno 'lima' linaweza kutumika kuunda maneno mengine katika Kiswahili k.m mkulima, kilimo, nimelima, limika n.k Katika kubadilisha mofimu hizi, tunaweza kubadilisha neno moja kutoka aina moja(kitenzi) hadi nyingine (nomino) n.k
 7. Sintaksi - (au sarufi miundo) ni tawi la isimu au taaluma ya sarufi inayoshughulikia jinsi vikundi vya maneno na sentensi mbalimbali zinajengwa katika lugha. Sintaksia huangazia kanuni au sheria za lugha. Kila lugha huwa na sheria zake za kuambatanisha maneno kama vile jinsi ya kufuatanisha vitenzi, nomino na vielezi. Kwa mfano: Mtoto yako shiba ni sentensi isiyokuwa na sintaksi. Sentensi sawa ingekuwa: Mtoto wako ameshiba.
 8. Semantiki - ni tawi la isimu linalochunguza maana halisia (mantiki) ya maneno, kifungu au sentensi katika lugha. Sentensi isiyokuwa na mantiki ni sentensi inayotoa maana ambayo haiwezekani katika uhalisia. Sentensi inaweza kuwa sawa kisintaksia lakini iwe na makosa ya kimantiki. Kwa mfano: Kiatu cha mbwa kimefutwa kazi kwa sababu kumi ni kubwa kama hewa.

Aina za Lugha Katika Isimu Jamii

 1. Lafudhi - Ni upekee wa mtu katika matamshi (accent) unaoathiriwa na lugha ya mama, mazingira yake ya kijiografia au kiwango ujuzi wake wa lugha.
 2. Lahaja - ni vijilugha vinavyoibuka kwa lugha moja kuu kutokana na tofauti za kijiografia baina ya wazungumzaji wa lugha hiyo. Kwa mfano lugha ya Kiswahili ina lahaja kadhaa kama vile Kimtang'ata, Kilamu, Kimvita, n.k. Tofauti baina ya lufudhi ni kama msamiati, muundo wa sentensi au matamshi.
 3. Lugha rasmi - ni lugha inayotumika katika shughuli za kiofisi ama ya wakati wa mawasiliano rasmi katika taifa fulani. Kwa mfano, lugha rasmi nchini Kenya ni Kiingereza.
 4. Lugha rasimi - ni mtindo wa lugha uliotumiwa na mtu/watu fulani mashuhuri (zamani) na ambao huonekana kuwa mtindo bora wa lugha unaofaa kuigwa na wengine. Kwa mfano lugha ya Shakespeare.
 5. Lugha ya taifa - ni lugha inayoteuliwa na taifa fulani kama chombo cha mawasiliano baina ya wananchi, kwa maana inazungumzwa na wananchi wengi katika taifa hilo. Lugha ya taifa, nchini Kenya ni Kiswahili; Uganda ni Kiganda.
 6. Lugha Sanifu - Ni lugha iliyokarabatiwa na sheria zake (k.v muundo wa sentensi, msamiati, sarufi, n.k) kubainishwa na kuandikwa, na kwa hivyo huzingatia sarufi maalum na upatanisho sahihi wa sentensi. Kwa mfano: Kiswahili sanifu - ni lugha isiyokuwa na makosa ya kisarufi.
 7. Lingua Franka - Ni lugha inayoteuliwa miongoni watu wenye asili tofauti wasiozungumza lugha moja ili iwe lugha ya kuwaunganisha katika shughuli rasmi au za kibiashara.
 8. Pijini - ni lugha inayozaliwa kutokana na mchanganyo wa lugha zaidi ya moja. Kwa mfano. Sheng' (lugha ya vijana mitaani nchini ni lugha iliyoibuka kutoka kwa Kiswahili na Kiingereza.
 9. Krioli - Ni pijini iliyokomaa na kukubalika.
 10. Lugha mame - hii ni lugha isiyokua na ambayo hubaki kati umbo lake la awali. Kwa mfano lugha ya Kilatini haibadiliki na hivyo hutumika katika kubuni majina ya kisayansi, n.k.
 11. Lugha azali - ni lugha inayozaa lugha nyinginezo.
 12. Misimu - ni lugha yenye maneno ya kisiri ambayo hutumiwa na kikundi fulani cha watu katika jamii, inayoeleweka tu baina yao. Misimu huibuka na kutoweka baada ya muda.

93 Comments


Guest Mgeni - Mar 08 2013, 4:52am

asante

Guest Mgeni - Mar 09 2013, 8:52am

tafadhali nipe mifano ya nomino mahususi

Guest Mgeni - Mar 11 2013, 5:08am

Tafadhali naomba mfano wa maneno ya kimvita.

Guest Mgeni - Mar 15 2013, 2:39am

kiswahili damu na litukuzwe
gor mahia htdhdtrjdtdjffjfgfjdy

Guest Mgeni - Mar 15 2013, 2:39am

Masalaale!!!! Ebo!! Gai wakwa!! huu ni Kiswahili sanifu sana hadi na elewa kila kitu!!
AFC Leopards

Brian Yego - Mar 18 2013, 8:35am

ninashukuru sana kwa sababu ya hii paneli.

Amos kinuthia - Mar 21 2013, 2:01am

hii paneli imekikuuza kiswahili changu sana.ashanteni.lakini ningewaomba pia muongeze vitabu vya fasihi kama utengano na vya riwaya

alexander mulu - Apr 01 2013, 1:28am

pokeeni kongole zangu nyote mnaochangia katika kukuza lugha yetu tukufu ya kiswahili.

Richie Richard - Apr 01 2013, 4:03am

Kwa kweli,lazima nipite kiswahili.sioni mbona nianguke.

mutua yule mmoja - Apr 03 2013, 3:35am

tuendeleeni kukuza na kuiendeleza lugha ya kiswahili kwani ata wale wanaiona kama lugha duni wanaitumia kila siku katika shughuli zao.

Oscar Ochieng' N. - Apr 04 2013, 3:12pm

Shukrani chekwa.
Inna Kiswahili kidumishwe.

Joshua mchokozi - Apr 08 2013, 4:23pm

Paneli inafanya vizuri hasa kwa wanafunzi

Iddah John - Apr 10 2013, 5:36am

paneli iboreshwe kwa sababu inasaidia katika kukuza na kuendeleza lugha hii ya kiswahili

Joseph mwachi - Apr 12 2013, 8:22am

Nini umuhimu wa fonolojia na fonetiki kwa mwalimu wa kiswahili.

ADAMSON - Apr 20 2013, 3:11am

kimatamshi NA lafudhi

HELENA GERALD - Apr 22 2013, 3:57am

isimu jamii ina mawanda mapana ...jadili""

mercy massawe - Apr 23 2013, 3:19am

ni kweli isimu jamii ina mawanda mapana kwani taaluma ambayo ina jihusisha na taaluma nyingine nyingi kama vile sosiolojia, saiklojia na nyingine nyingi.

lubale - Apr 26 2013, 6:45am

baini makosa yoyote kifonimu katika matamshi ya konsonanti
-lubale barasa

Moses - Jun 01 2013, 7:53am

Naomba wanaochangia ukurasa huu wakosolewe. Baadhi yao wanatumia kiswahili kiholela hasa ngeli. Wengine pia wanaokana kukidharau kiswahili jinsi wanavyopachika maneno ovyo. Asiyejua ngeli hajui kiswahili.

MURUNGI NICHOLAS - Jun 06 2013, 8:58am

Nawapa mkono wa tahania nyie nyote mnaochangia kuikuza lugha yetu teule ya kiswahili

MSUVA WISLEN - Jun 09 2013, 9:40am

Kiswahili ni lugha yetu, hatuna budi kujisifu kwayo yatupasa kwa juhudi zote tuikuze ili ifikie hadhi ya juu kabisa kimataifa kama kilivyo kiingereza

MSUVA WISLEN - Jun 09 2013, 9:40am

Kiswahili ni lugha yetu, hatuna budi kujisifu kwayo yatupasa kwa juhudi zote tuikuze ili ifikie hadhi ya juu kabisa kimataifa kama kilivyo kiingereza

Dennis Mutai - Jun 09 2013, 10:04am

kazi njema kabisa lakini pia ningependa kuona jukumu la mofolojia katika kuchangia matawi hizo zingine za fonetiki, fonolojia, semantiki na kadhalika

Mearcy Lonney - Jun 13 2013, 2:27am

Kazi njema lakini mbona hakuna mwongozo wa kuandika insha ya ripoti?

Peter sagini - Jun 14 2013, 12:54pm

Kutoka st vincent ninashukuru sana katika bahari ya fasihi

MSUVA WISLEN - Jun 15 2013, 8:01pm

Nahitaji dua na sala zenu ndugu zangu nataka kuandika kitabu cha kiswahili kinacho husu lugha ya kiswahili na lugha za afrika kwa ujumla.kama una ushauri kwangu waweza wasiliana nami kupitia emaili yangu wislenmsuva@gmail
.com au namba ya simu 0759930143

SOLO YEGON - Jun 17 2013, 1:20pm

hongera kwa paneli ya kiswahili, naomba usaidizi wenu kujibu swali hili: UKUBWA WA NENO MWALIMU ni nini?

DUNCAN MWILARIA NGATUNYI - Jun 22 2013, 2:03pm

Kongole mabingwa.

watuwa shaban - Jun 25 2013, 3:25am

tafadhali naomba nielezewe mahusiano ya kisema
ntiki

Omunyin peter - Jun 28 2013, 7:37am

Mwanafunzi wa shule ya upili ya wavulana Kolanya. Pögezi,kazi nzuri kabisa.

Geoffrey - Jun 29 2013, 2:34am

nashukuru kwa mchango wenu kwa kupiga hatua kwa kiswahili nawashukuru

Anuarite - Jul 16 2013, 11:28pm

Hi ni paneli nzuri, lakini weka mahali Watusi wanauliza maswali na hujibiwa saa hiyo hiyo

Anuarite - Jul 16 2013, 11:29pm

Nilitaka kusema watu. Ni komputa yangu.

MMASI PHILIP - Jul 24 2013, 10:55am

KAMA MWALIMU MTARAJIWA WA KISWAHILI NANUFAIKA SANA .TUENDELEE KUKIKUZA KISWAHILI.

kithi francis - Jul 29 2013, 12:55pm

Tofauti za kifonolojia na kimsamiati katika lugha ya kiswahili:kiamu,kipate,kimtangata

hezron morang'a - Aug 05 2013, 3:37am

jadili ni kwa nini lugha ni mali ya binadamu.

MURIU EVANSE M - Aug 20 2013, 12:32pm

Hongera kwa kazi nzuri!

Maryam suleiman - Aug 21 2013, 7:14pm

Eleza vile lugha inaweza kutumika kuleta maridhiano miongoni mwa watu wanaozozana.

FREDRICK ODHIAMBO OCHIENG - Aug 23 2013, 7:18am

Tafadhali wanaochangia kwa kutoa maoni wakikuze kiswahili kwa kutumia lugha sanifu .Hata hivyo hongera kwa wale wote walio na matumaini kwamba kiswahili bado kina nafasi ya kuboreka zaidi na wanaziunga juhudi hizo za kukiboresha zaidi. Hatimaye naomba kupewa sifa za sajili ya matatu na za sajili ya magazetini.

Michael onyango - Sep 01 2013, 9:41am

Hongera kwa kazi nzuri.

Ogina - Sep 02 2013, 4:14pm

Hongera sana kwa mabingwa wa jopo hili teule kwa ajili ya kiswahili, labda kuwapa tu motisha, kama mpenzi wa lugha hii nikotayari na pamoja nanyi kwendeleza kazi hizi. Bw. Ogina Owollah

Ogina - Sep 02 2013, 4:16pm

Ahsanteni wanajopo kazi yenu yaonekana wazi

Patrick Mutinda - Sep 04 2013, 4:30am

Nataka kujua uhusiano wa isimu na historia,sayansi, sosholojia na pia jiografia.

Jacinta Kagendo Magaju - Sep 04 2013, 2:25pm

Nawahongera wanalugha wenzangu kwa ukwasi walio nao. Wanafunzi wa ngazi zote watafaidi.
Kiswahili kitukuzwe!

korir kiprono denis - Sep 18 2013, 3:20am

Asante! ningependa kupata ufafanuzi zaidi kuhusu sintaksia.

sally chepwogen - Oct 05 2013, 2:18pm

tofautisha maneno yafuatayo: foni,fonimu ,alofoni ,mofu , alomofu ,mofimu.

Winnie Lukungu - Oct 10 2013, 8:44am

Kwa hakika nimenufaika sana na sehemu hii. Hongera.Nami pia nitajahidi angaa nichangie jambo. Bi.Winnie-Shule ya upili ya Wavulana-Kangundo.

Mw. Abondo - Oct 14 2013, 12:47pm

Sally, ningependa kukupa mwogozo wa swali lako. Kidogo muda umenizonga.
japo pia Mkuu wa wavuti hii, hajatupa sehemu ya kutoa maoni yetu kifasili.

Stella wanja - Oct 15 2013, 9:49pm

Shukran za dhati mabingwa. Ningewaomba wanaotoa mchango wao wazingatie sarufi.

gideon katumo - Oct 16 2013, 3:51am

nawapa mkono wa tahania nyie wapenzi wa kiswahili. ndio, kiswahili kitukuzwe.

gideon katumo - Oct 16 2013, 4:28am

nawaomba tafadhali ndugu wapenzi na mahiri wa lugha ya kiswahili mnisaidie hapa: fafanua uhusiano uliopo kati ya taaluma ya isimu na taaluma nyingine kama vile; historia, saikolojia, anthropolojia, ufundishaji na sosholojia

collin nyandiwa - Oct 21 2013, 3:16am

naomba mfano wa shairi ya ngonjera. Asanteni

Rodgerson Gisemba Rajah Mosoti - Oct 30 2013, 9:15am

Kazi yenu ni nzuri. Endeleeni vivyo hivyo.

Omonge Kenneth Omonge - Nov 01 2013, 6:34am

Ningependa kunyosha mkono wangu kwa washika dau kwa vile jitihada zao zimekuwa kama gunzo katika usanifishaji wa lahaja mbalimbali ili kupata lugha ya kiswahili sanifu.

benard seroney - Feb 11 2014, 2:04am

ngeweza kuuliza ya kwa wakati unatarajiwa kufunza kidato cha kwanza utatumia mbinu gani ya kufunza ili waweze kuelewa kwa undani....

benard seroney - Mar 01 2014, 4:09am

heei! wenzangu hakuna yule angeweza kunipa jawabu la swali hili? tufanyaje basi iwapo sipati jibu..........?

mutharimi Zablon - Mar 11 2014, 2:22am

Asanteni sana Kwa paneli hii imenisaidia sana Kwa maswali mengi , hongera!

mutharimi Zablon - Mar 11 2014, 2:29am

bwana bernard , jibu ukonalo wewe mwenyewe , wewe umefusu kuwa mwalimu mwenye shaada katika shule Za upili lazima utumie mbinu zote zile umefudishwa kushughulikia wanafunzi wa Kila kiwango.

David Kamau - Apr 02 2014, 1:11pm


David Kamau - Apr 02 2014, 1:12pm

Vyema endeleeni vivyo hivyo......Mola ambariki

Mkissi Mmoja Yule - Apr 05 2014, 10:28am

Kiswahili kitambae. Hongera

Francis ekai - Apr 17 2014, 6:46am

Kongole kwa lugha na saha ya kiswahili tafathali nawezanje kupata makaratasi ya KCPE Kudurusu tafadhali

vilsack ogari - Apr 22 2014, 2:47am

kongole enyi wote mnao changia kwa kushamirisha kiswahili

EJIDIO MAINA - Apr 22 2014, 8:23am

TAFADHARI NIELEZE UMUHIMU WA ISIMU JAMII

Geol - Apr 28 2014, 7:06am

Nadharia za isimu jamii ndio zipi

Lennah Kinoti - Apr 28 2014, 8:52am

Nielezee yafuatayo:a]mambo yanayoathiri matumizi ya lugha katika jamii
b]lugha ni nini
c]majukumu ya lugha katika jamii

joel mubweka - May 04 2014, 1:43am

Tafadhali nadharia za isimu jamii ndizo zipi

ISAAC NAMBANGA - May 05 2014, 9:50am

KISWAHILI kitukuzwe siku zote. Nii mwanafuu katika shule ya upili ya nambale. Ninajivunia sana lugha kiswahili .

ISAAC NAMBANGA - May 05 2014, 9:52am

KISWAHILI kitukuzwe siku zote. Nii mwanafuu katika shule ya upili ya nambale. Ninajivunia sana lugha kiswahili .

SALIHA Y. MSUYA - May 19 2014, 1:46pm

Safi sana. Fafanua sintakisia ndugu

isaac wanyoike - Jun 08 2014, 5:31am

Nawashukuru sana kwa kazi yenu swafi, hongera.

John - Jun 24 2014, 4:48am

wapo wanaosema kuwa Lingua Franka ni lugha ya kwanza inayobuniwa wakati watu wa asili tofauti wanapotangamana. je, falsafa hii ni sahihi?

MARTIN - Jul 01 2014, 3:04am

MAMBO YANAYODHIBITI LUGHA KATIKA JAMII

peninah kangwony - Jul 11 2014, 9:57am


peninah kangwony - Jul 11 2014, 9:59am

shukrani kwa kazi njema

AUGUSTINE KIRIMI IRITI - Jul 15 2014, 9:17am

LUGHA BANDYA NI IPI?

Hassan Hussein - Jul 21 2014, 4:20pm

Asalam aleyqum...Nawaombeni mtubainishie sifa za lugha rasmi, ya kitaifa na kimataifa... hata hivyo asanteni kwa kutuelimisha.

bonface murimi - Jul 23 2014, 11:26am

hongera magwiji wa lugha

vivian - Jul 29 2014, 12:11pm

Fafanua maana na tofauti kati ya uhonominia na upolisemia

gahungup - Aug 15 2014, 2:17pm

kweli tunashukuru sana jinsi munatuelimisha.Endelea na kuboresha mambo yenu.Mungu muumba azidi kuwapa neema kutoka kwake.

Joseph Mutemi - Aug 18 2014, 10:42am

asanteni kwa kukituza kiswahili

nasia - Aug 19 2014, 9:44am

wacha wapenzi wa kiswahili tujivunie kwa kukiongea nakukiandika kila wakati,tuzindue na kuwavumbua macho ndugu zetu waliopotea

bisharo - Aug 26 2014, 2:07pm

kazi nzuri

Wanjala Lennox - Sep 24 2014, 11:47pm


Wanjala Lennox - Sep 24 2014, 11:48pm

shikilia hapo magwiji.

Wanjala Lennox - Sep 24 2014, 11:49pm

shikilia hapo magwiji.

Ong'ayi J Benson - 6 weeks ago

Nawashukuru sana,naomba usaidizi,"jadili jinsi lugha ya kiswahili ilivyoenea nchini kabla ya kupata uhuru"

Samwel Oluoch - 5 weeks ago

Kongole kwa maelezo haya azizi.Swadakda.

jared mesa mirieri - 5 weeks ago

Maelezo mema ila tunahitaji mifano katika dhana ulizozieleza hapo juu.Ikiwezekana sana tutungie kitabu nakiwepo madukani.Nitafurahi sana ikiwa ombi langu litashughulikiwa nawe/nanyi.Na kama kipo nitashukuru ikiwa mtanijulisha anwani yacho ndipo nipatenakala yangu mwenyewe.Tuzidi kwa moyo mkunjufu kukipigania Kiswahili ndipo nacho kiwe na nafasi kubwa katika jamii ila tusiche tukawa tunatawalwa na ubinafsi katika huimalishaji wake.KEN WALIBORA-"Sisi ni wajenzi wa nyumba moja, mbona tupiganie fito?"SHUKRAN SANA MAFARISI.

Kassim Zagu Haji - 4 weeks ago

Sio mbaya kazi yako ila ungejaribu kuonesha pia malengo ya isimu jamii pamoja na jinsi inavyohusiana na taaluma nyengine.Asante kwa kazi nzuri.

kanyi - 4 weeks ago

Hongera sana kwa ufafanuzi wenu.ningependa pia mnisaidie kutofautisha tanzu nne za kisarufi ambazo uwiano na uchanganuzi wa kifonologia

abdullahi kheyrow Noor - 3 weeks ago

Hongera kwenu

Gerry - 2 weeks ago

Swadakta....maelezo ya kina wakereketwa

Login to Comment