Nimtume Nani


By Fr. D. Ntampambata

Nimtume Nani Lyrics

  NIMTUME NANI

  Nimtume nani?
  Unitume mimi nitume Bwana
  (Nita) Nitakwenda kutangaza Neno lako Bwana
  Mataifa ya dunia yakufuate wewe
  Unitume mimi nitume Bwana

 1. Bwana asema, Nimtume nani
  Aende kuwahubiria mataifa?
 2. Bwana amenituma kuihubiri,
  habari njema kwa watu;
  Roho wa Bwana yu juu yangu
 3. Kwa maana amenitia mafuta
  Kuwahubiria maskini habari njema

  Bwana ndiye kiongozi wangu
  Anisaidie kuchunga neno lake


  < Alternative stanzas>

 4. Mkingali tumboni mwa mama zenu
  naliwatakasa, nalikuita ili uwe mtume wangu.
 5. Mtakwenda kutangaza neno langu,
  msiogope kwa ajili ya hao.
 6. Mimi katika mashaka na shida zao zote,
  mimi nitawafundisha mtakayosema

Comments