Nikulipe Nini


By Alfred Ossonga

Nikulipe Nini Lyrics

 1. Nikulipe nini ewe Mungu Baba wa Mbinguni
  Kwani mtu mimi sina kitu cha kujivunia

  Uhai na nguvu ni zawadi nzuri umenipa wewe Baba.
  Maisha mazuri ni talanta safi nimepata kwako wewe
  Sasa nakuomba baba nigeuze chombo chako
  Nimejitolea kwenda kutangaza neno lako *2

 2. Nikufananishe na nini humu ulimwenguni
  Uliumba vyote bahari mito hata milima
 3. Ningekuwa ndege hakika ningeruka angani
  Ningekuwa nyota ningemulika dunia yote
 4. Nitakutendea nini ili nikufurahishe,
  Nitakuimbia wimbo gani Baba nikusifu
 5. Unitume Baba popote nipeleke ujumbe
  Nitalihubiri Jina lako daima milele

Comments