Moyo Wangu Wamtukuza


By Fr. G. F. Kayeta

Moyo Wangu Wamtukuza Lyrics

  {(Moyo) Moyo wangu wamtukuza Bwana
  (Roho) Roho yangu inafurahi }*2

 1. Kwa kuwa amemwangalia, kwa huruma mtumishi wake
  Hivyo tangu sasa watu wote, wataniita mwenye heri
 2. Kwa sababu Mwenyezi Mungu, amenifanyia makuu
  Jina lake ni takatifu,
 3. Huruma yake ni kwa wote, wote wale wanaomcha
  Kizazi hata na kizazi,
 4. Huyatenda mambo makuu, kwa nguvu za mkono wake
  Wenye kiburi hutawanywa,
 5. Hushusha wote wenye vyeo, kutoka vitini vya enzi
  Nao wale wanyenyekevu, wote hao huwainua
 6. Huwashibisha wenye njaa, na matajiri huwaacha
  Waende mikono mitupu,
 7. Hulilinda taifa lake, teule la mtumishi wake
  Akikumbuka huruma yake,
 8. Kama alivyowaahidia, babu zetu kuwaahidia
  Ibrahimu na mzao wake,
 9. Atukuzwe Baba na Mwana, naye Roho Mtakatifu
  Leo kesho hata milele, kwa shangwe milele amina

  ~Lk. 1:39-55

Comments
Sauti Tamu
St. Paul's Students Choir is launching an app through which customers can order, pay and receive their music through their smart phones or choir website . You can get lyrics, mp3s and videos, for all our albums. Try the app Sauti Tamu mobile app.

A new approach to spread the gospel to all nations. The app also supports automated music sales for M-Pesa (Kenya and Tanzania).

Try it today! Perhaps this is what you/your choir has been looking for!