The largest library of songs from East African Catholic community with over 1440 entries. Nyimbo za kwaya mbalimbali za kikatoliki kutoka Afrika Mashariki.


Sauti za Kuimba ni talanta tumepewa na Mungu
Ni talanta, tutumie watu waokolewe, wauone uso wa Mungu
Tuwafariji waombolezao, tuwape tumaini walokata tamaa
Tuwateteee wasio na mtetezi, walionyamazishwa na kelele za dunia
Tuwaburudishe waliozubazwa na taabu za dunia


Sauti za Ngoma. Sauti ya kinanda. Sauti ya kinubi. Sauti ya kayamba. Sauti ya zeze. Sauti za Ala Zote za Muziki. Pamoja na sauti tamu tulizojaliwa. Hizi ni Sauti za Kuimba.


Nyimbo za Advent na Christmas Noel
Request for Lyrics here.


Kinukuu Teule


Nimetafakari habari zako nami nashindwa kuelewa kabisa
Binadamu angenipa neema kesho angechoka kunipa zaidi
Lakini wewe hauna kikomo, wala mvua yako haina majira
Bwana, wanyesha mvua, Bwana, kwa walio jangwani
Bwana, wawasha jua, Bwana, mpaka baharini
Kweli Bwana wewe ni mwema sana


Yesu ni Mwema - B. Mukasa

Hubirini kwa Sauti ya Kuimba, tangazeni haya, yatamkeni mpaka mwisho wa dunia